​DAWATI LA JINSIA LATAKIWA KUANDAA MPANGO KAZI WA KURATIBUSHUGHULI ZAKIJINSIA WIZARANI.

Imewekwa: Thursday 22, April 2021

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Imani Kapinga amelitaka dawati la waratibu wa dawati la uvuvi la jinsia la wizara ya mifugo na uvuvikuhakikisha wanaandaa mpango kazi ambao utabainisha shughuli mbalimbali zinazohusu masuala ya kijinsia.

Dkt. Kapinga ametoa kauli hiyo wakati akifungua warsha ya mafunzo ya waratibu wa dawati la uvuvi la jinsia la Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayofanyika Mkoani Morogoro Aprili 21-23/2021.

Amesema mafunzo hayo wanayoyapata ni muhimusana katika kujenga uwezo wa utekelezaji wa mpango kazi ambao utaongeza ufanisi katika dawati na kuwataka kuwa wasikivu ili kufikia malengo tarajiwa.

“Baada ya mafunzo haya tunaanza mpango kazi ambao utabainisha shughuli mbalimbali za kijinsia na hii itasaidia sana kuongeza ufanisi wa dawati lakini pia kuongeza ujumuishi wa masuala ya jinsia katika shughuli za wizara za kila siku” amesema Dkt. Kapinga.

Dkt. Kapinga ameongeza kuwa Serikali inatambua kuwa karibia asilimia 98 ya wavuvi nchini ni wavuvi wadogo hivyo serikali iliamua kuanza kutekeleza mwongozo wa hiari kwa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu.

Alisema kupitia mradi huo wa mwongozo wa hiari, maeneo yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na uanzishwaji wa jukwaa la wanawake yaani Tanzania Women Fish Workers Association (TAWFA) lililozinduliwa mwaka 2018.

"ili kuwezesha ufanisi wa jukwaa hili la wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi nchini ndio dawati la jinsia la uvuvi lilianzishwa pamoja na mambo mengine, najukumu lenu kubwa ni uratibu wa jukwaa hilo la wanawake. “ amesema Dkt Kapinga.

Warsha hiyo ya siku tatu ambayo lengo lake ni kutoa mafunzo ya waratibu wa dawati la Uvuvi la jinsia la Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayofanyika Mkoani Morogoro imefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wa EAF Nanseni.

.